Wewe Mungu Twakukiri (Te Deum)
Ki: Wewe, Mungu twakukiri
Wewe, Bwana wa Milele,
Wewe, Bwana wa Milele,
Ush: Ulimwengu wote unakuabudu.
Ki: Malaika wote wakusujudia Wewe.
Ush: Nazo Mbingu na Nguvu zote;
Ki: Nao makerubi na maserafi wakuimbia hawakomi:
Ush: Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, BWANA
Mungu wa majeshi,
Ki: Mbingu na nchi zimejaa utukufu wako.
Ush: Jamii tukufu ya Mitume wakusifu Wewe;
Ki: Shirika lenye sifa la manabii wakusifu Wewe.
Ush: Jeshi la Mashahidi waliovaa mavazi muepe wakusifu wewe;
Ki: Kanisa takatifu katika nchi zote lakukiri Wewe;
Ush: Baba mwenye enzi zote; Mwana wako pekee,
na wa kweli, wa kuabudiwa; Mfariji Roho Mtakatifu.
na wa kweli, wa kuabudiwa; Mfariji Roho Mtakatifu.
Ki: Wewe Kristo ndiwe Mfalme wa Utukufu,
Wewe Mwana wa milele wa Baba.
Ush: Hata ulipowadia utimilifu wa wakati wa kuwaokoa binadamu,
Ulichukua mwili huu wetu katika tumbo la Bikira Mariamu.
Ki: Wewe ulipoushinda uchungu wa mauti,
Uliwafungulia waaminio Ufalme wa Mbinguni.
Ush: Wewe unakaa mkono wa kuume wa Mungu katika utukufu wake Baba.
Ki: Tunaamini na kungojea kurudi kwako kuwa mwamuzi wetu.
Ush: Kwa hiyo twakuomba uwasaidie watumishi wako.
Ki: Watumishi hawa uliowakomboa kwa damu yako ya thamani,
Ush: Uwajalie pamoja na watakatifu wako
Thawabu ya utukufu wa milele. Amen.
Uwaokoe watu wako, Bwana: uubarikie urithi wako.
Uwatawale: uwainue hata makao ya milele.
Sisi kila siku: twakutukuza.
Twalisifu Jina lako: zamani hizi na za tnilele.
Ukubali, Bwana, kutulinda leo: tusipate dhambi.
Uturchemu, Bwana: umrehemu sisi.
Utuonee huruma, Bwana: kwani sisi twakutumaini wewe.
Nirnekutumaini wewe, Bwana: nisipotee milele.
The last 8 lines are reproduced from: INJIA Y A IBADA. Swahili: Book of Worship SOCIETY FOR PROMOTING CHRISTIAN KNOWLEDGE. LONDON: p. 3-4]
https://docplayer.net/53409897-Njia-y-a-ibada-swahili-book-of-worship-society-for-promoting-christian-knowledge-njla-ya-ibada-book-of-worship-london.html]