Friday, October 05, 2018

'Bokoreri Obuya Nkorw' Asore: Ekegusii hymn

The Music Teacher from Lutheran Theological Seminary-Nyamira, Kenya with his family singing the first two verses of hymn 70 from the Ekegusii hymnal Moterere Omonene.

'Bokoreri Obuya Nkorw' Asore, 
lyrics by Enock Kalembo
1. Omo:
'Bokoreri obuya nkorw' asore,
Omonene bw'obonene.
Ring'ana rigiy' erieta riao.

Bonsi:
/:Yeso nomochakano bw'emeremo,
na nechinguru ase obokoreri bwaito.:/

2. Omo:
Abakoreri mogondo oo,
obae ososemeria.
Ne chinguru kobr' emeremo.

Bonsi:
/: Bakore yonsi ase obwegenwa,
bab' abarendi eri' emeremo tesareka. :/

Enock Kalembo's Kiswahili version is #71 in Mwimbiene Bwana

Wednesday, October 03, 2018

Kiswahili Te Deum Wewe Mungu Twakukiri-Draft

This is for the proof-readers, a draft engraving of the first setting of the Te Deum (p. 383-384) in the Kiswahili hymnal Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! This hymnal was produced in 2000 by the Evangelical Lutheran Church in Tanzania. 
Wewe Mungu Twakukiri (Te Deum)


Ki: Wewe, Mungu twakukiri
Wewe, Bwana wa Milele,
Ush: Ulimwengu wote unakuabudu.


Ki: Malaika wote wakusujudia Wewe.
Ush: Nazo Mbingu na Nguvu zote;


Ki: Nao makerubi na maserafi wakuimbia hawakomi:
Ush: Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, BWANA
Mungu wa majeshi,


Ki: Mbingu na nchi zimejaa utukufu wako.
Ush: Jamii tukufu ya Mitume wakusifu Wewe;


Ki: Shirika lenye sifa la manabii wakusifu Wewe.
Ush: Jeshi la Mashahidi waliovaa mavazi muepe wakusifu wewe;


Ki: Kanisa takatifu katika nchi zote lakukiri Wewe;
Ush: Baba mwenye enzi zote; Mwana wako pekee,
na wa kweli, wa kuabudiwa; Mfariji Roho Mtakatifu.


Ki: Wewe Kristo ndiwe Mfalme wa Utukufu,
Wewe Mwana wa milele wa Baba.
Ush: Hata ulipowadia utimilifu wa wakati wa kuwaokoa binadamu,
Ulichukua mwili huu wetu katika tumbo la Bikira Mariamu.


Ki: Wewe ulipoushinda uchungu wa mauti,
Uliwafungulia waaminio Ufalme wa Mbinguni.
Ush: Wewe unakaa mkono wa kuume wa Mungu katika utukufu wake Baba.


Ki: Tunaamini na kungojea kurudi kwako kuwa mwamuzi wetu.
Ush: Kwa hiyo twakuomba uwasaidie watumishi wako.


Ki: Watumishi hawa uliowakomboa kwa damu yako ya thamani,
Ush: Uwajalie pamoja na watakatifu wako
Thawabu ya utukufu wa milele. Amen.


Uwaokoe watu wako, Bwana: uubarikie urithi wako.
Uwatawale: uwainue hata makao ya milele.
Sisi kila siku: twakutukuza.
Twalisifu Jina lako: zamani hizi na za tnilele.
Ukubali, Bwana, kutulinda leo: tusipate dhambi.
Uturchemu, Bwana: umrehemu sisi.
Utuonee huruma, Bwana: kwani sisi twakutumaini wewe.
Nirnekutumaini wewe, Bwana: nisipotee milele.

The last 8 lines are reproduced from: INJIA Y A IBADA. Swahili: Book of Worship SOCIETY FOR PROMOTING CHRISTIAN KNOWLEDGE. LONDON: p. 3-4]

https://docplayer.net/53409897-Njia-y-a-ibada-swahili-book-of-worship-society-for-promoting-christian-knowledge-njla-ya-ibada-book-of-worship-london.html]

Saturday, September 29, 2018

Kiswahili Invocation -- Draft

This is for the proof-readers, a draft engraving of the first setting of the Invocation in the Kiswahili hymnal Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! This hymnal was produced in 2000 by the Evangelical Lutheran Church in Tanzania.


I Maandalio: Ungamo na Ondoleo la Dhambi (MB p. 267)

Invocation

Ki: Kwa Jina la Mungu Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.

Ush: Amen.WIMBO


Ki: Bwana Mungu wetu yupo hapa, yu pamoja nasi. Tumsujudie, tumche. Na tumsikie jinsi anavyotufundisha katika Neno lake:

ama: Mpende Bwana Mngu wako kwa moyo wako wote, na wka roho yako yote, na kwa akili zako zote; Mpende na jirani yako kama nafisi yako.

au: Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine ila mimi. Usilitaje bure Jina la Bwana Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. Ikumbuke siku ya Bwana, uitakase. Waheshimu Baba yako na Mama yako. Usiue. Usizini. Usibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usitamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake, wala ng’ombe wake, wala chochote alicho nacho.

Ki: Msaada wetu ni katika Jina la Bwana,
Ush: Aliyeziumba mbingu na dunia.


Friday, September 28, 2018

Kiswahili Gloria In Excelsis Second Version -- Draft

This is for the proof-readers, a draft engraving of the first setting of the Gloria in Excelsis in the Kiswahili hymnal Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! This hymnal was produced  in 2000 by the Evangelical Lutheran Church in Tanzania.Twakusifu (Gloria in Excelsis) Njia ya pili [Second Version] 

Thursday, September 27, 2018

Kiswahili Gloria In Excelsis First Version -- Draft

This is for the proof-readers, a draft engraving of the first setting of the Gloria in Excelsis in the Kiswahili hymnal Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! This hymnal was produced  in 2000 by the Evangelical Lutheran Church in Tanzania.


UTUKUFU NI WA MUNGU (Gloria in Excelsis)Text Criticism News

Ancient History and Archaeology