Saturday, September 29, 2018

Kiswahili Invocation -- Draft

This is for the proof-readers, a draft engraving of the first setting of the Invocation in the Kiswahili hymnal Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! This hymnal was produced in 2000 by the Evangelical Lutheran Church in Tanzania.


I Maandalio: Ungamo na Ondoleo la Dhambi (MB p. 267)

Invocation

Ki: Kwa Jina la Mungu Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.

Ush: Amen.



WIMBO


Ki: Bwana Mungu wetu yupo hapa, yu pamoja nasi. Tumsujudie, tumche. Na tumsikie jinsi anavyotufundisha katika Neno lake:

ama: Mpende Bwana Mngu wako kwa moyo wako wote, na wka roho yako yote, na kwa akili zako zote; Mpende na jirani yako kama nafisi yako.

au: Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine ila mimi. Usilitaje bure Jina la Bwana Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. Ikumbuke siku ya Bwana, uitakase. Waheshimu Baba yako na Mama yako. Usiue. Usizini. Usibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usitamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake, wala ng’ombe wake, wala chochote alicho nacho.

Ki: Msaada wetu ni katika Jina la Bwana,
Ush: Aliyeziumba mbingu na dunia.